Ili uweze kuikuza biashara yeyote ile unatakiiwa kuwa na nidhamu sana katika mauzo yako. Bila kuwa na nidhamu binafsi katika mauzo yako kuna uwezekano mkubwa biashara yako ikafa mapema zaidi.
Jambo la kuzingatia ni kuwa ili biashara yako isife mapema unatakiwa kuhakikisha kuwa kiasi kikubwa cha faida unayoipata katika biashara yako unairudisha tena kwenye biashara hiyo.
Ukiendelea na utaratibu wako wa kutumia faida yote unayoipata kwenye biashara yako lazima biashara hiyo itakufa tu, itakufa kwa sababu biashara itakuwa haikui.
Pia siku zote tunaambiwa ukuaji wa biashara yeyote ile inategemea na matumizi ya faida sahihi inayopatikana kwenye biashara husika.
Sasa kazi ibaki kuwa kwako kuanzia leo, kwamba ili uweze kukua zaidi katika biashara yako unatakiwa kurudisha faida unayoipata kwenye biashara yako. Ukifanya hivi ni lazima tu utaona unakuwa kila siku.
Tunataka kusikia kutoka kwako kwamba ulianza na mtaji wa elfu moja ila baada ya muda fulani mtaji wako ni laki moja, hili linawekana kabisa, hivyo kazi ibaki kuwa kwako kwenye utekelezaji wa kurudisha faida unayoipata kwenye biashara.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments