Nguvu pekee ambayo unapaswa kuiwekeza katika biashara yako ili uweze kuuza zaidi biashara yako, unatakiwa kuwekeza muda wako mwingi kujifunza ushawishi.
Ushawishi wako ndiyo ambao humsadia mteja aweze kununua bidhaa yako. Kama utakuwa huwezi kushawishi wateja zako kununua kile unachokiuza hakuna kitu ambacho utaweza kukiuza.
Mara nyingi amini kuwa mteja hana nguvu kubwa ya kununua kitu akitakacho kama wewe muuzaji utakuwa huna nguvu ya kumshawishi.
Hivyo ni jambo jema kuwekeza nguvu yako kubwa kwenye kushawishi wateja wako ili uweze kuuza zaidi. Mteja yeyote anayekuja kuhitaji huduma yako usimuache aende bila kununua, mshawishi mpaka anunue.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments