Changamoto kubwa ambayo wafanyabiashara wengi wameikumbatia kwa muda mrefu na bado wanaendelea kuibeba ni pamoja na kuendelea kuangalia mauzo zaidi badala ya kuangalia faida.
Kwa mfano, wengi wao husema leo nimeuza mauzoya elfu hamsini na kusahau kuangalia faida itokanayo na mauzo hayo ya shilingi elfu hamsini. Wengi huweka mauzo na faida kama ni kitu kimoja kitu ambacho siyo sahihi hata kidogo.
Kitendo hiki cha kuangalia mauzo kama faida kimewafanya watu wengi biashara zao zife kwa sababu wamekuwa hawaelewi kama wanakula mtaji bila wao kujua kwa sababu wao huangalia mauzo badala ya kuangalia faida.
Ikiwa na wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia hii ya kuangalia mauzo badala ya faida unapaswa kuanzia leo kuubadili mtazamo wako utakaokusaidia kutofautisha kati ya mauzo na faida.
Kwenye kila mauzo yako unapaswa kujua faida ni ipi, ili ujue namna sahihi ya kutumia faida hiyo kwa maendeleo yako binafsi na biashara kiujumla. Ukifanikiwa katika hili utaona biashara yako inakua na utazidi kusonga mbele kila uchwao.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments