Unapoanza kufanya biashara yeyote ile unatakiwa kuwa makini sana katika namna sahihi ya kuindesha biashara hiyo, kwani kama hautakuwa makini huenda biashara hiyo isiwe na maisha marefu ya uwepo wake tokea kuanzishwa kwake.
Hii ni kwa sababu mara nyingi biashara mpya huwa zina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wateja wengi wanakuwa hawajakufahamu hivyo mara nyingi huwa hawana uhakika na wewe kwenye kile unachokiuza.
Pamaja na hayo ili uweze kukua zaidi katika biashara hiyo mpya uliyoianzisha au unayotaka kuianzisha unatakiwa sana kuepuka kutumia faida unayoipata kwenye matumizi mengine ambayo yapo nje na malengo ya biashara yako.
Kwa maneno mengine tunaweza kusema ili uweze kukua katika biashara yako mpya basi asilimia kubwa ya faida unayoipata katika biashara yako basi hakikisha unairudusha katika biashara yako ili uweze kukuza mtaji wako.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments