BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo la kujifunza kutoka kwa William Shakespeare.



William Shakespeare anatukumbusha mimi na wewe ya kuwa katika ulimwengu si kila mtu wa kumwamini kwa asilimia zote, kwa sababu sisi binadamu hatufanani tabia na mawazo, unaweza kumuamini mtu, lakini mtu huyo huyo akaja kukuumiza na kuliza mbeleni.

Kwa nukta hiyo william shakespeare anatukumbusha kuwa tunapaswa kuwapenda watu wote, Ila linapokuja suala  la kuamini tunapaswa kuwaamini watu wachache. Tunapaswa kuwaamini watu wachache wenye akili timamu ambao hawatakuwa vyanzo vya maumivu mbeleni. 

Ni muhimu kuamini watu wachache maishani mwetu ili kupunguza maumivu na gharama sizizokuwa na tija, kwa sababu kama tutawaamini watu wote ni lazima maumivu mbeleni yatakuwa ni makubwa tu na muda wakuweza kuyatatua maumivu hayo utakuwa ni mwingi zaidi. Penda wote, amini wachache.

Post a Comment

0 Comments