BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo la kujifunza kutoka kwa Confucius.

Confucius aliwahi kusema kuwa mara nyingi ugumu wa maisha sisi wenyewe ndiyo chanzo cha ugumu huo. Confucius anasema mara nyingi tunafanya vitu kwa mazoea sana na baadae tunakuja kulalamika kuwa maisha ni magumu.

Confucius anasema maisha ni marahisi sana endapo tuatacha kufanya vitu mbalimbali vyenye kuleta tija kwa mazoea. Confucius anasema kama kweli tunataka kubadili matokeo ya yale tuyafanyayo basi tuache kufanya mambo kwa mazoea kwani kufanya vitu vya mazoea tutaendelea kupata matokeo yale yale tuliyoyazoea kuyapata. 

Hivyo ni jambo lenye kuleta tija maishani endapo tutaamua kuyabadili maisha yetu kutoka kuwa magumu na kuwa mepesi kwa kuepukana kufanya vitu kwa mazoea ili tuweze kupata matokeo tofauti.

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp, au BONYEZA HAPA mafanikioapp@gmail.com kuwasiliana nasi kupitia email kwa ajili ya Maoni, Ushauri, Mapendekezo au  Changamoto.

 


Post a Comment

0 Comments