BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Dunia Inapoamua Kukufundisha...

Dunia inapoamua kukufundisha jambo haisemi kwa sauti na wewe, inakufundisha kimya kimya, lakini utaelewa ina maanisha nini, hata kama unajifanya kiziwi, ila utaelewa.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uishi kwa NIDHAMU, haisemi na wewe kwa sauti, matokeo ya kutokuishi na NIDHAMU utayaona, kama kweli hutaishi kwa NIDHAMU.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uishi kwa UADILIFU, haisemi na wewe kwa sauti, matokeo ya kutokuishi kwa UADILIFU utayaona wewe na jinsi yatakavyokugharimu.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa UJITUME, haisemi na wewe pia kwa sauti hata kidogo, bali matokeo ya kutokujituma utayapata na kutakuwa hakuna wa kumlaumu hata mmoja.

Dunia inapoamua kukufundisha ya kuwa uwe na matumizi mazuri ya pesa, haisemi na wewe kwa sauti, kama unaamua kutumia pesa hovyo, we tumia, siku ukija kuzikosa utajuta sana.

Dunia inapokufundisha kwa chochote, haisemi kwa sauti, haigombani na wewe, ni wewe tu unatakiwa uwe makini na lugha ambayo dunia inasema na ufuate maelekezo hayo.

Kama usipoweza kuisikiliza dunia inasema nini na wewe kwenye maisha yako, basi utaharibu sana maisha yako. Mambo mengi utayavuruga kwa sababu huisikilizi dunia.

Dunia inasema na wewe, unatakiwa kuweka masikio yako kuisikiliza. Kama utaisikiliza vizuri na kwa umakini, basi utaweza kufanikiwa. Kama usipoweza, utapotea.

Ukikosea katika kuisikiliza dunia, basi utaharibu sana maisha yako na utakuwa na maisha ya hovyo. Jambo la muhimu kwako, ni kuwa makini na kuisikiliza dunia, hapo utafanikiwa sana.

BONYEZA HAPA 👉 https://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia whatsApp.

 

Post a Comment

0 Comments