Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye kipindi cha hedhi hukumbwa na tatizo la kwenda haja kubwa mara kwa mara au pia kuhara (kuharisha). Hali hii ni kawaida, siyo tatizo.
Hutokana na sababu mbili ambazo ni kushuka kwa kiasi cha homoni za progesterone kwenye damu na kuongezeka kwa homoni za prostaglandins kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ambazo huufanya uzidishe mawimbi ya miondoko yake kuelekea chini (sehemu ya haja kubwa).
Hali hii haihitaji dawa,huisha yenyewe tu baada ya kufikia ukomo kwa hedhi ya mwezi husika
Imeandikwa na Dk. Harun Mmari
Kama unahitaji ushauri wowote wa masuala ya afya tafadhari wasiliana naye kwa nambari 0625-940497
0 Comments