BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya homa ya ini aina "E" inavyosababishwa

 


Aina E ya homa ya Ini husambazwa kupitia maji machafu,hasa kwenye maeneo yenye usafi duni. Vinyesi vyenye virusi hawa vilivyo changanyikana na maji yanayotumiwa na watu ndiyo chanzo kikubwa cha kutokea kwake.

Aina hii ya homa ya Ini ni hatari sana kwa wanawake wajawazito hasa walio kwenye kipindi cha pili na tatu cha ujauzito kwani huweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito, kushindwa kufanya kazi kwa ini na wakati mwingine husababisha kifo.Asilimia 20-25 ya wanawake wajawazito hupoteza maisha ikitokea kwa bahati mbaya wameshambuliwa na aina hii ya homa ya ini.

Nini cha kufanya? Pima afya yako,kama utakuwa hujaathirika na changamoto yoyote ya Homa ya Ini pata chanjo. Kama umeathirika basi pata tiba.
Homa ya Ini ni hatari!

IMEANDIKWA NA DK. HARUN MMARI
0625-940497


Post a Comment

0 Comments