BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo yanayotuchelewesha sana katika kuyasaka mafanikio

Miongoni mwa mambo yanayotuchelewesha sana katika kuyasaka mafanikio yetu ya kila siku ni pamoja na kuwa navisingizio vingi, wapo baadhi ya watu wao ukiwauliza ni kwanini maisha yao ni ya kawaida,wengi wao watakupa visingizio visivyokuwa vya msingi. 

Kwa mfano wapo baadhi ya watu wao husema kwamba, wao ni maskini kwa sababu hawajasoma, wengine eti kwa sababu wametoka familia maskini pamoja na visingizio vingine kama hivyo.

Hivyo endapo tunayo nia ya kweli katika kuyasaka mafanikio ambayo yatakuwa na faida kwetu, ni lazima tutafuta njia ya kuyafikia mafanikio hayo, ila kama hatuna nia ya  kweli katika kuyasaka mafanikio ni kwamba tutafuta visingizio visivyokuwa na lazima.

Ili kupata matokeo chanya katika maisha yako, amua sasa kubadilika kwa kuanza kutafuta njia za kutafuta njia zitakazo kupeleka kwenye mafanikio. Achana na tabia ya kutafuta viisngizio visivyokuwa msingi  na lazima.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
0757909942

Post a Comment

0 Comments