Kila mwanadamu ameumbwa
na kusudio lake hapa dunia. Pia itakuwa ni dhambi kubwa kama upo hapa
duniani pasipo kutambua hilo kusudio lako.
Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika yale wayafanyayo hii ni kwa sababu
watu hao wanafanya vitu ambavyo sio vyao bali ni vya watu wengine.
Watu wengi tunaishi kwa
kuigaiga mambo ya watu wengine, yaani utakuta mtu fulani anafanya jambo fulani
kisha mtu mwingine naye anaanza kufanya jambo hilo , kitendo hiki ni kujipoteza
wewe mwenyewe pasipo wewe kujua kwa sababu hicho siyo kitu chako.
Hivyo
zifuatazo ndizo kanuni za kujua kusudio la kuumbwa kwako;
1.
Muombe
mwenyezi Mungu.
Kwa imani uliyonayo basi
unashauriwa kutumia imani hiyo hiyo kuomba Mungu akujalie ili uweze kufahamu
kusudio lako la uwepo wako katika sayari hii. Kwani ukweli ni kwamba Mungu wetu ni
mwema na ni muaminifu pia, hivyo tunaamini anatambua kila mmoja wetu lengo lake
ni nini hapa duniani.
2.
Hakikisha
unafanya kitu ambacho unakipenda.
Miongoni mwa mambo ambayo
humsaidia mtu ili aweze kujua lengo lake na kuwepo hapa duniani ni pamoja na
kufanya mambo ambayo anayapenda.
Wengi wetu tunashindwa
kufanikiwa katika maisha hii ni kwa sababu tunafanya vitu tusivyovipenda. Hivyo
kila wakati unatakiwa kuhahakisha kila unachokifanya unakipenda kutoka moyoni
mwako.
Kama unafanya jambo ambao
hulipendi unashauri uachane na jambo hilo mara moja kwani ni sawa na kupoteza
muda tu, kwani unatakuwa unafanya ilimradi siku iendee tu.
3.
Jitafute/wewe
ni nani?
Unashauriwa pia ili uweze
kutambua uwezo ulionao ni pamoja na kuwekeza muda mwingi wa kujitafuta wewe ni
nani. Ninapozungumzia wewe ni nani hapa ni maana ya kwamba ni lazima uwaze kuwa
wewe upo vizuri katika kufanya jambo gani?
Mara baada ya kupata
majibu ya kwamba wewe upo vizuri katika jambo gani ndipo unapotakiwa kuwekeza
nguvu, muda, akili na pesa katika kulitekeleza jambo hilo.
Kama wewe ni
mwanamitindo, mfanyabiashara, fundi au jambo lolote lile basi ni vyema ukaweka
mkazo wa kiutendaji katika mambo hayo na si vinginevyo.
Pia ni ili uweze
kujitabmbua wewe ni nani zinahitajika akili za ziada za kuweza kujitambu
madhaifu na uwezo ulionao katika utendaji wa jambo Fulani.
Katika madhaifu uliyonayo
basi yafanyie kazi madhaifu hiyo ili weze kuondokana nayo kabisa, ila katika
uwezo ulionao basi unatakiwa kuongeza juhudi ili uweze kufanya bora zaidi ya
uwezo wako.
Hayo ni baadhi ya ya mambo
ya msingi unayopaswa kuzingatia katika kutambua kusudio lako hapa dunia ili
uweze kuishi maisha yenye furaha hatimaye kupata mafanikio unayoyataraji.

0 Comments