Kwenye maisha haya ya kila siku, endapo utawekeza akili yako katika kutegemea na kuamini katika matokeo yaliyo chanya pekee ni kwamba ni lazima utashindwa tu katika mambo yako hata iweje, hii ni kwa sababu kila jambo ambalo leo hii limekuwa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa basi jambo hilo lilipitia changamoto nyingi sana ndani yake.
Hivyo hata wewe usitegemee kwamba mafanikio unayotafuta hayana changamoto kitu hicho hakipo, Ikumbukwe kwamba kila kitu chenye mafanikio kimeambatana na changamoto ndani yake.
Hivyo usiwe muoga wa kuogopa ugumu na changamoto zitakazojitokeza kwenye kile ukifanyacho, bali unatakiwa kuelewa changamoto ni njia sahihi zitakazokusaidia kukupeleka katika mafanikio yako endapo utafuta majibu sahihi ya changamoto hizo.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
0757-909942
bensonchonya23@gmail.com

0 Comments