BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kanuni Sita (6) Muhimu Za Mafanikio.

Leo nitaomba nichukue walau dakika chache ili niweze kukumbusha kanuni sita za kukupa mafanikio unayoyahitaji, na kanuni hizo ni kama ifutavyo.


1. Miongoni mwa vitu vitakuvyofanya uzidi kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa ni pamoja na kuendelea kuchukua hatua stahiki kwa hicho unachokifanya au kile unachotaka kufanya.


2. Mafanikio ni mataokeo ya vile unavyoitumia siku yako vyema, hivyo ulivyo leo ni matokeo ya hatua ulizozichukua siku ya jana. Hivyo jifunze kuitumia leo yako vyema ili uishe kesho yako yenye mafanikio na furaha tele.


3. Hivyo ulivyo leo katika suala la mafanikio hutokana na mawazo yako, kama mawazo yako ni hasi basi hata maisha yake yatakuwa vivyo hivyo, hivyo ili kuweza kuishi maisha yenye mabadiliko makubwa unatakiwa kushughulika na mawazo yako ipasavyo yaani kila wakati unatakiwa kubadili mtazamo wa vile unavyoamini.


4. Kama tutaamua kutafuta mafanikio ya kweli ni lazima tutafuta njia ya kuyapata mafanikio hayo, ila kama hatuhitaji mafanikio ni lazima tutafuta visingizio. Hivyo ili tuweze kufika katika kilele cha mafanikio tunatakiwa kutafauta njia ya kuapata mafanikio hayo.


5. Katika maisha haya kila kitu kinawezekana, kama kuna jambo unaliona ni changamoto na haliwezekani basi mahala hapo ndipo palipo na fursa lukuki zilizojificha, hivyo jifinze kushughulika na kila changamoto zilizopo katika jamii yako kwani hapo ndipo palipo na fursa.


6.  Inaelezwa kuwa siraha hatari zaidi duniani si bunduki wala mabomu ya nyuklia kama wengi wadhanivyo, bali siraha hatari zaidi duniani ni hofu. Hofu ndio chanzo kikubwa cha kuuwa ndoto za walio wengi, wengi wetu tunashindwa kuthubutu kufanya jambo fulani eti kwa sababu ya kwamba tunaogopa kitu fulani.

Hivyo kama kweli unataka kupiga hatua za kusonga mbele tunatakiwa kuhakikisha ya kwamba tunaondokana na hofu, kwani hofu ni adui nambari moja wa mafanikio.


Asante sana kwa kusoma makala haya kupitia mtandao huu wa Mafanikio App, nikutakie siku njema na mafanikio Mema.


Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya

mafanikioapp@gmail.com


Post a Comment

0 Comments