BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze kufanya kile unachokipenda ili kupata matokeo makubwa

Kila wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya kile unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa. Kupenda kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni rahisi tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’ hasa kama unafanya kile unachokipenda. 

Mara nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

dirayamafanikio@gmail.com


Post a Comment

0 Comments