Mara zote tunakumbushwa
ya kwamba ajianavyo mtu ndivyo alivyo. Miongoni mwetu tumekwisha kukataa tamaa
ya maisha kabisa, wengi tumeshapoteza matumaini kwa kiwango kikubwa, hatuamini
kama ipo siku ambayo tutatafanikiwa, wengi tumejione hatuna mamlaka ya kupata
kile tunachokitaka.
Na hali hii imejitokeza
ndani yetu baada ya kuanza kuishi mawazo ya watu wengine, wengi tumekuwa
tukiwatazama wengine hasa pale ambapo wameshindwa hivyo, kujiona ya kwamba na
sisi hatuwezi. Ila ninachotaka kukwambia ya kwamba kushindwa kwa wengine liwe
somo kwako ili uweza kufanikiwa zaidi.
Hii ni kwa kwa sababu
hali yoyote ile ambayo inatoka nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza
kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho
kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.
Hali hiyo inayotokea
ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako. Hebu
jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba
utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Ni vyema kutafakari hivyo
kwa sababu haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu
dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi
huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa,
lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio basi ni lazima utafanikiwa.
Kitu kikubwa hapa
unachotakiwa kujifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha
yako kwamba ndio imekukwamisha. Hii ni
kwa sababu wengi wetu ni wazuri sana katika kulaum watu wengine ya kwamba wao
wamesababisha wewe kuwa hivyo ulivyo leo na
inawezekana sababu hiyo ukaiona ina mashiko sana kwa upande wako, ila
ninachopaswa kukwambia ni nyanyuka upya kwa kuanza kufikiri upya na pia dawa ya
wapuuzi ni kuwapuuza.
Nasema hivyo kwa
sababu anakuzuia kupata mafanikio yako
ni wewe mwenyewe pamoja na mawazo hasi unayozidi kuyabeba kila wakati. Narudia
kusema tena uduni wa maisha yako hausababishwi na mtu mwingine bali wewe mwenyewe. Hivyo ni
jambo lenye busara sana ambalo ni vyema kuanzia leo, amua kujenga hali bora
ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
Hivyo ni malize kwa
kusema ya kwamba huwezi kutokea kwa jirani bila kuanzia kwako, hii nikiwa na
maana acha kulamu watu wengi anza kuona maisha yako mkoseaji mkubwa ni wewe ni
si mtu mwingine, hata kama ni kweli mtu mwingine ndiyo sababu yaw ewe kuwa
hivyo ulivyo ninachotaka kukusihi ni kwamba ni tafauta mbadala wa kutatua changamoto
inayokukabili na si kuwa walaam watu wengine.
Asante kwa kuwa msomaji
wetu wa mtandao huu wa dira ya mafanikio nakusihi uwashirikishe na wengine
kadri uwezavyo.
Imeandikwa na
uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio na Mafanikio App
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya
0 Comments