Kwa
kawaida, yapo mambo manne tu ambayo yanafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa,
lakini si hivyo tu hayo ndiyo ndiyo mambo ambayo karibu maskini wote duniani
wanayafanya sana maishani mwao. Na kwa kuendelea kufanya mambo hayo iwe kwa
kujua au kutokujua ni chanzo kikubwa sana cha kuvuta umaskini kila iitwapo leo.
Ikiwa hata wewe utaendelea kufanya mambo hayo sahau kutoka kwenye umaskini, hata
ufanyaje utaendelea kubakia hapo.
1. Kulalamika.
Watu
wengi tumekuwa ni wazuri sana katika kona hii, hata kwa vitu ambavyo tunavimudu.
Ulamikaji huu huenda sambamba na visingizio ambavyo kwa upande chanya havina
mashiko kabisa, Hata hivyo inasadadikia
ya kwamba walalamikaji wengi huwa ni ngumu kufanikiwa katika maisha yao, chunguza
hilo kisha uone ukweli juu ya jambo hili.
Endapo
utachukua jukumu la kuwauliza watu wengi ni kwa nini wanakuwa hivyo walivyo
leo, majibu yao unaweza sema labda dunia haina usawa, kumbe ukweli ni kwamba
hakuna aliyewahi kependelewa katika dunia hii, kwa sababu katika sayari hii
vitu vilivyopo vipo sawa kwa ajili ya watu wote. Hebu tazama masaa wote tuna
masaa sawa. Sasa utafauti wetu unakuja wapi?
Ukweli
ni kwamnba utofauti wetu unakuja pale ambapo tunakuja kuyatumia masaa haya,
hapo ndipo yanapatengenezwa yale makundi mawili ya waliyonacho na wasionacho.
Hivyo ili tuweze kutengeneza makundi sawa ya walinacho pekee, tunachotakiwa
kufanya na kuacha kulalamika hasa kwa mambo ambayo hayana msaada wowote katika
maisha yetu.
2. Kulaumu wengine.
kama wewe ni mtu wa kulaumu wengine kwa kila
kitu na kujiona ni mtu wa kutokosea , sahau kutoka kwenye umaskini. Huu ni
kweli ambao upo wazi, kwa sababu watu wengi tupo katika maisha ya kawaida kwa
sababu ya kukaa na kulaam watu wengine. Kufanya hivi ni kulisindikiza jua
kutimiza wajibu wake. Kwa kila kitu ambacho unakifanya acha mara moja
kunyooshea kidole watu wengine na badala yake unachotakiwa kufanya fanya kazi
kama vile dunia hii unaishi pekee yako.
3. Kutokuwajibika katika maisha yako.
Hutakiwi kulaumu serikali, ndugu, jamaa au
wazazi wako ya kwamba wao ndio wamefanya maisha yako yawe hivyo. Wewe ndiye mtu
wa kwanza wa kuwajibika na maisha yako. Hivyo unachotakiwa kufanya kila wakati
ni kuhakikisha unatoa maaumuzi sahihi hasa katika maisha yako. Hata kama dunia
nzima haita tambua mchango wako,
mathalani wewe unajua ni nini ambacho unakitaka basi nakusihi uendelee kupana
mpaka tone la mwisho.
4. Kutokuwa na shukrani.
Hiki
ni kipimo tosha kwamba unafanikiwa au hufanikiwi. Kama huna shukran hata kwa
kidogo unachopata, mafanikio makubwa kwako itabaki hadithi. Hivyo kwa kila
wakati jambo la kwanza unalopaswa kulipa kipaumbele ni ile hali ya kuwashukuru
watu wote walifanikisha wewe kuwa hapo ulipo ukianza na mwenyezi Mungu, kisha watu wengi ndiyo wafuate.
Tunakutakia
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa..
Ndimi Afisa Mipango Benson chonya
0747-030303
mafanikioapp@gmail.com
0 Comments