BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 


Kitabu kizuri na bora katika maisha bado hakijaandikwa mpaka muda huu.

Wimbo mzuri na pengine kuliko nyimbo zote pia bado haujaimbwa duniani.

Mwandishi bora wa makala na mwandishi wa vitabu pia bado hajatokea na kuandika.

Mjenzi mzuri wa maghorofa, na majengo makubwa makubwa, bado pia hayupo.

Chakula kizuri na chenye radha safi na bora, bado hakijapikwa na mpishi yeyote yule.

Machine nzuri ya kisasa na mashine pengine yenye maajabu bado haijavumbuliwa.

Mauzo makubwa katika biashara na yenye faida, bado hayajafanyika popote pale.

Na mfanyabiashara mkubwa wa kupindukia na kuweka rekodi nzuri zaidi bado pia hajatokea.

Yale mafanikio makubwa unayoyaona katika dunia ya leo, ni ishara tu kwamba kuna mafanikio makubwa zaidi na ya kupindukia yanakuja.

Mafanikio hayo makubwa yajayo hayapo kwa mwingine bali kwako. Tambua kila mtu ndani yake ana mbegu za mambo makubwa, kazi yako ni kuzikuza.

Ubora wa maisha yako na maisha ya wengine na kufanya mambo yawe makubwa upo ndani yako. Una subiri nini, chukua hatua na fanya mambo makubwa.


Post a Comment

0 Comments