Kwa chochote ufanyacho, jitahidi sana ufanye kwa ubora, kama hautafanya kwa ubora basi unajidanganya mwenyewe, maana ni lazima utashindwa. Ubora ndio silaha kubwa ya kukufikisha kwenye mafanikio.
Fanya kwa ubora kwa wengine. Fanya kwa ubora kwa wateja wako, rafiki zako na hata ndugu zako. Kila eneo ukifanya kwa ubora, mafanikio kwako itakuwa ni kitu cha kawaida, maana ni lazima utafanikiwa.
Zipo fursa nyingi sana ambazo zinatakiwa kufanyika kila siku. Fursa zote hizo zinahitajika kufanya kwa ubora ili kuweza kufanikiwa sana. Kama kutakuwa hakuna ubora, mafanikio yanakuwa hayapo ya uhakika.

0 Comments