Kitu kigumu kuliko mafanikio yenyewe, ni jinsi ya kulinda mafanikio hayo uliyoyapata. Kuna watu ambao wanajua vizuri juu ya kutafuta mafanikio yao, lakini linapokuja suala la kuyalinda mafanikio ili yadumu, hapo tena linakuwa shida kwao. Utashangaa kila kitu kinaanza tena kupotea.
Kwa mfano, utakuta mtu amefanikiwa kupata pesa kiasi fulani kwa shida sana, tena mtu huyo anakuwa wa kwanza kuzitumia hovyo. Si hivyo tu, yapo maeneo mengi ambayo watu wanafanikiwa lakini wanashindwa kuyalinda mafanikio hayo. Jifunze kulinda mafanikio yako kuanzia sasa ili upige hatua zaidi.

0 Comments