BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Kila siku mpya kwako, unatakiwa ujue inaweza kuwa ni fursa kubwa ya kuweza kutengeneza au kufanya maisha yako kuwa bora zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kuitumia siku yako vizuri sana, ili uweze kufikia mafanikio yako.

Leo ni siku ambayo unatakiwa uitumie  kuongeza juhudi kidogo zaidi ya jana, unatakiwa pia ufanye kwa ubora kuliko jana na pia uweze kujitoa kuliko jana. Ukifanya hivyo, ipo nafasi kubwa ya wewe kuweza kufanikiwa.

Ikiwa kuna kitu unataka kukibadili, basi elewa kabisa leo ndio siku ya kufanya hivyo. Hutakiwi kuanza kesho au wiki lijalo, anza leo kukibadili kitu hicho mara moja. Ukiitawala leo yako vizuri, UMEFANIKIWA.


Post a Comment

0 Comments