Ili uweze kufanikiwa katika maisha zipo hatua ambazo unalazimika kupitia hadi kufanikiwa. Ikiwa utaruka hatua hizo utakuwa unajidanganya mafanikio hutayaona. Kwani hiyo itakuwa ni sawa na mmea ni lazima upande, upalilie hadi kuvuna.
Tatizo la watu wengi wanataka mafanikio ya haraka sana. Utakuta mtu kaanzisha kitu leo anataka kilete mafanikio kesho. Watu hawa wanakuwa ni sawa na mtu anayepanda leo halafu kesho anakwenda kuangalia kama anaweza akaanza kuvuna.
Maisha ya mafanikio kwa ujumla yanapitia kwenye mchakato, hakuna mafanikio ya ghafla ambayo unaweza ukayapata. Ni muhimu kuweza kujipa muda ambapo huo muda utakusaidia kuweza kutimiza malengo yako.
0 Comments