BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Chamcha na Robert Kiyosaki.

Naitwa Benson mjukuu wa mzee Robert Kiyosaki, ukiniliuliza Robert kiyosaki na babu yako mzaa nani?, jibu langu ni babu yangu mzaa mafanikio ya wengi hasa wale wasomao na kuyaishi maandiko yake.

Siku ya leo nilipata nafasi ya kula chakula cha mchana na babu yangu mwandishi Robert Kiyosaki. Wakati tumemaliza kula aliniambia vitu vingi sana, lakini kitu hiki ndicho ambacho hakinitoki akilini.

Mzee wangu Robert kiyosaki alisema, Benson mjukuu wangu  "mara nyingi ukiiruhusu akili yako isema kwamba siwezi kufanya kitu hiki, akili nayo huamua kulala kwa sababu hata wewe mwenyewe umekili kwamba haiwezekani".

"Ila  kama utairuhusu akili yako iwaze ni kwa namna gani utaweza kufanikisha jambo fulani, akili nayo huingia kazini kuwaza namna ya kufanikisha jambo hilo". 

CHAMCHA maana yake ni Chakula cha mchana

Na; Beson Chonya, Afisa Mipango! 


Post a Comment

0 Comments