Jaribu kujiuliza ni kitu gani, ambacho unaweza ukakifanya pasipo ya wewe kushindwa. Jibu lake, ni HAKUNA. Kila kitu utakachokifanya ni lazima utashindwa kwa namna moja au nyingine, hilo liko wazi.
Ikiwa wewe unaogopa kuchukua hatua kwa kuogopa kushindwa, naomba nikwambie tu umechemka, tena sana tu umechemka. Kushindwa kupo pale pale, hata uchukue tahadhari kubwa vipi.
Hivyo, wito wangu kwangu kwako, ni kukwambia wewe amua kuchukua hatua, ukishindwa, basi kubali kujifunza na songa mbele. Usikubali hapo ulipo kwa kuogopa eti utashindwa, utajidanganya etii.
Imani Ngwangwalu.
0 Comments