Ni watu wachache sana, ambao wana uwezo wa kupiga hatua kubwa na kufikia mafanikio yao mara moja, lakini watu wengi wanachoweza kufanya ni kuchukua hatua ndogo ndogo, hadi kufikia mafanikio yao.
Angalia maisha yako, kuna wakati unaona unakutana na changamoto kubwa sana, lakini kwa kadri unavyopambana na changamoto hizo zinazidi kuwa ndogo na unaona sio changamoto tena.
Kuna kitu ambacho unaweza ukakifanya leo, kesho au wiki lijalo, lakini kitu hicho kikawa kidogo tu, lakini cha kuboresha maisha yako. Acha kuwaza kupiga hatua kubwh sana, hatua ndogo pia zitakufanikisha.
Imani Ngwangwalu.
0 Comments