BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo


Kama hujachukua hatua ya kuelekea kwenye ndoto zako, basi elewa hutaweza kufanikisha chochote. Kama utaendelea kushangaa watu wanavyofanya piga hatua, utabakia hapo ulipo yaani utakuwa msindikizaji tu.

Unachotakiwa kufanya ni kuruka hapo ulipo kwenye kushangaa na kuchukua hatua. Lazima uchukue hatua ili kutimiza ndoto zako. Usijali hatua utakazochukua, hata kama ni hatua kidogo, lakini chukua hatua.

Safari ya kufikia mafanikio yako sio rahisi. Ndio maana wabeba vyuma, hawafanikiwi kwa kubeba vyuma vyepesi, kuna kazi inahitajika kufanyika ili kufanikiwa. Unatakiwa uchukue hatua za kubadili maisha yako.

Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments