Leo ni siku muhimu sana kwako. Ninasema leo ni siku muhimu kwako, nikiwa na maana, siku kama hii ya leo, ikipita kwenye maisha yako haitakuja kutokea tena siku kama hii milele maishani mwako. Kwa kujua hilo hii ni siku ambayo, unatakiwa uifanye iwe bora sana, kwa kufanya yale yaliyo bora na kuipa umuhimu wa pekee.
Kila muda au saa katika siku hii ya leo, unatakiwa ulifanye liwe kama dhahabu kwako. Kila saa katika siku ya leo, linatakiwa liwe ni saa la kujifunza, kukua, kutengeneza thamani, kutengeneza utajiri na kufanya mabadiliko kwenye maisha yako na maisha ya wengine.
Kile utakachokifanya leo kwa ubora, kitaboresha maisha yako ya kesho. Kile utakachokifanya leo kwa ubora, kitabadilisha dunia yako. Leo ni siku bora ya ufunguo wa mafanikio yako. Fikiri, kama usipoifanya leo kuwa siku muhimu, siku ya mabadiliko yako, unafikiri itakuwa lini?
Kuna yale mambo ambayo ulikuwa ukiyatamani kuyafanya, hebu amua kuyafanya leo katika siku hii muhimu. Kuna zile ndoto ambazo ulikuwa ukiziota na kutaka kuzitimiza, hebu zifanye leo hii. Leo iwe ndio siku ya wewe kuchukua hatua ya kwanza. Acha kusubiri kitu, leo ni siku yako muhimu ya kufanya mabadiliko chanya ya maisha yako ya leo na ya baadae ikiwa utaamua kweli.
Leo ni siku moja ya muhimu sana kwako. Ifanye iwe siku ya mabadiliko makubwa kwako. Hutakiwi kulaza damu zaidi ya kuchukua hatua kwenye siku hii ya leo. Je, uko tayari kuifanya siku ya leo kuwa muhimu kwako na kukubali, kujifunza, kukua, kutengeneza thamani, kutengeneza utajiri na kufanya mabadiliko ya maisha yako na wengine? Naamini uko tayari...
Imani Ngwangwalu
0 Comments