BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze haya kutoka kitabu cha "The Power of a Positive Mindset: Transform Your Mind, Transform Your Life" kilichoandikwa na Jason Wolbers

 


Hapa kuna mafundisho 5 kutoka kitabu "The Power of a Positive Mindset: Transform Your Mind, Transform Your Life" kilichoandikwa na Jason Wolbers:

1. Kuwa na mtazamo chanya: Mwandishi anaeleza kwa kina kabisa kuhusu umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, huku akituasa kuwa na mtazamo chanya kunasaidia sana kuweza kuvuka kwenye changamoto mbalimbali zinazotukabili. Pia kuwa na mtazamo chanya kunasaidia kujifunza zaidi, vilevile hutusaidia kuona changamoto kwenye jicho la fursa.

2. Kuaiamini nafsi yako: Wolbers anasisitiza sana umuhimu wa kuamini katika mawazo yako ni chachu ya mafanikio unayoyataka. Kila upatapo mawazo chanya yaamini mawazo hayo kisha mawazo hayo yabadili katika matendo ili uweze kupata kitu halisi. Usipoweza kuyaamini mawazo yako hata mawazo ya watu wengine huwezi kuyaamini pia, hivyo anza kuamini mawazo yako kuanzia sasa.

3. Kuza mtazomo chanya: mwandishi anasisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya. Mtazamo chanya kujengwa na kujifunza vitu kila wakati, unapojifunza vitu kila wakati kuna kusaidia kutoka kwenye tatizo la msongo wa mawazo na hivyo unakuwa mtu mwenye mtazamo chanya utakaokupa mawazo waweshi yenye kukupa maendeleo uyatakayo.

4. Jifunze kujinenea maneno chanya: mwandishi Wolbers anahimiza umuhimu wa matumizi ya maneno chanya ambayo unajinenea kila wakati. Kila wakati hakikisha unajinenea maneno mazuri na chanya ambayo yatakupa nguvu na hamasa ya kufanya yaliyo na mafanikio zaidi. Epuka kujinenea maneno ambayo yatakutisha tamaa, maneno kama mimi siwezi na mengine mengi yanayokutisha tamaa hayapaswi kuwa upande wako.

5. Kukuza mtazamo wa ukuaji: mwandishi anahamisisha kila mmoja awe na mtazamo wa ukuaji, ambapo anasema mtazamo wa ukuaji ni kama vile kukubali changamoto, kuyapokea maoni ya watu wengine yatakayotusaidia kuwa bora zaidi na zaidi lakini pia mwandishi anatuasa sana tuwe tayari kujifunza mambo mapya yatakayotusaidia kuweza kuwa bora zaidi.

Kikubwa ambacho mwandishi amelenga kwenye kitabu hiki ni kuwahamasisha wasomaji kuwa na mtazamo chanya, mtazamo ambao utakusaidia katika kukupa fikra chanya zitakazokusaidia kuweza kuzikubali changamoto na kujua mbinu sahihi za kuweza kujinasua katika changamoto hizo hatimaye kuweza kufikia mafanikio makubwa maishani.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments