BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kujifunza kutoka kwenye kitabu How To Attract Money cha Joseph Murphy.

 


Kitabu cha how to attract money kilichoandikwa na Joseph Murphy kinaleta mwanga na mafundisho muhimu kuhusu jinsi ya kuvuta pesa ili uweze kupata  utajiri katika maisha yako.

Yafuatayo ni mafundisho sita (6) muhimu kutoka kitabuni:

1. Kitabu kinaangazia juu ya suala ya mawazo na imani ya mtu binafsi kuhusu pesa. Ambapo mwandishi anatuasa tuweze kuwa na mtazamo chanya kuhusu pesa. Mtazamo huo ikiwa na pamoja na kuamini ya kuwa pesa ni zao litokanalo na kutoa thamani fulani.

Ili uweze kujenga mitazamo sahihi kuhusu pesa usiamini katika kutafuta pesa kwa kutumia nguvu za giza bali fedha huenda kwa mtu ambaye anatoa thamani fulani katika jamii. Vilevile pesa pesa huenda kwa mtu ambaye mara nyingi huwekeza katika juhudi zake katika kufanya kazi fulani. Kwa nukta hiyo mwandishi anatuasa sana kuwekeza katika kuamini kwenye mitizamo hiyo zaidi ili tuweze kuzivuta pesa zaidi.

2. Kujenga taswira ya kuwa tayari una miliki fedha. Mwandishi anatutaka  kufikiria kwa uwazi kuwa tayari unamiliki pesa unayoitaka na kuthibitisha taarifa chanya kuhusu utajiri huo wa kifedha, unaweza kuweka akili yako katika kujenga taswira hiyo kwani itakusaidia kupata fedha hizo. 

3. Sheria ya uvutano, kitabu kinajadili dhana ya sheria ya uvutano, ambayo inasema kuwa ili uweze kuzivuta pesa zije kwako unapaswa kuwa na vitu vikubwa viwili ambavyo ni kuwa na mtazamo chanya pia unapaswa kuwa mtu wa shukrani pia. Huwezi kufanikiwa kama hata kwa kile kidogo unachokipata huwezi kushukuru. 

4. Kuondokana na imani zinazopinga, wapo baadhi ya watu wamejijenga imani ambazo mara nyingi zinapinga kuhusu pesa. Wapo wale wanaoamini kuwa fedha zipo kwa ajili ya familia fulani pekee, kitu ambacho siyo kweli. Mwandishi anatutaka tujenga mitizamo chanya itakayotusaidia kuweza kuzivuta pesa. 

5. Kuchukua hatua  zitakazokusaidia kupata fedha zaidi. Kila wakati kuwa na mpango fedha, mpango ambao utakuwa kivitendo zaidi. Kama lengo ni kutengeneza laki moja kwa mwezi, basi yaweke wazi yale yatakayokusaidia kupata kile ulichokipanga. Weka pia mpango kazi ambao utakusaidia kwa kina kufikia kile unachokitaka, hayo si maneno yangu bali ya mwandishi Murphy.

6. Kila wakati jifunze kuzilinda rasimali ambazo zimekuwa zikukusaidia kupata fedha. Huwezi kuzivuta pesa kuja kwako kama vile vinavyokusaidia kupata pesa hizo huviheshimu. Pesa itaendelea kuja kwako kama utaendelea na suala la kuvilinda vile vitu vinavyokusaidia kuzipata pesa hizo.

Kwa leo naomba niishie hapo.

Ni mimi Afisa Mipango Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami

Post a Comment

0 Comments