BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mafunzo muhimu utayo jifunza Kwenye Kitabu "Psychology Of Money


Kitabu cha Physchology of money kikichoandikwa na Morgab Housel ni kitabu kizuri kinachoangazia elimu muhimu ya fedha. Kitabu hiki kimejaa mengi yatakayokuacha kinywa wazi kuhusu pesa. Miongo ni mwa mambo hayo ni pamoja na haya;

Usiwaoneshe watu wengine kama una pesa.
Mwandishi anatutaka tuache mara moja kuwaonesha watu wengine kama tuna pesa, hii kwa sababu wapo baadhi ya watu kila wapatapo pesa basi watataka kila mtu aone kama yeye ana pesa. 

Kutumia pesa kuonyesha watu kiasi cha pesa unacho ni njia ya haraka ya kuwa na pesa kidogo. acha maisha ya show off kwa sababu maisha haya huwafanya watu kuishiwa na pesa, kwani wengi wao huishi maisha yasiyo na uhalisia.

Thamani kila pesa inayopita mikononi mwako.
Acha mara moja tabia ya kutothamini pesa. Ukipata mia tano ithamini. Ipo nguvu kubwa sana ya kuthamini kila pesa unayoipata, hii kwa sababu kama utashindwa kuthamini kile kidogo ulichonacho basi hata ukipata kitu kikubwa utashindwa kukithamini vilevile.

Uhuru wa kifedha hutokana na kufanya kazi uipendayo.
Kama unataka kuwa na uhuru wa kifedha basi fanya kazi unayoipenda, ukifanya kazi unayouipenda utajitoa kwa moyo wako wote kwenye kazi hiyo kiasi cha kuwa na uchungu na kazi hiyo. Usiishie kufanya kazi unayoipendayo pekee bali fanya kazi na watu unaowapenda kwani kufanya hivi itakusaidia kupata matokeo sahihi pia.

Jifunze kuweka akiba.
Ugumu wa maisha usikutenge mbali na suala la uwekaji akiba. Kwenye kila kipato chako hakikisha unatenga walau kiasi fulani kwa ajili ya uwekaji wa akiba. Weka akiba kiasi kadhaa ambacho kwako utaona inafaa.

Kuwa mipango ni muhimu.
Fedha huenda kwa mtu mwenye mipango thabiti. Weka mipango thabiti ya kimaendeleo ambayo itakusaidia kupata fedha, kisha weka njia pia ya kukamilisha mipango hiyo. Kwa mfano kama lengo lako ni kutengeza shilingi 10,000 kila siku basi tengeneza mpango utakaokusaidia kupata kiasi hicho, kisha buni njia zitakazokusaidia kutengeneza kiasi hicho.

Kuwa na ratiba ya utendaji wa kazi zako.
Unapoianza siku yako usikurupuke bali jifunze kuwa na ratiba ya ufanyaji wa kazi, kazi ambazo zitakuongezea kipato. Kufanya kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba zako ni kupoteza muda. 

Yapo mengi ndani ya kitabu hicho cha cha saikolojia ya pesa, unachotakiwa  kifanya ni kutafuta kitabu hicho ili uweze kujisomea mwenyewe. 

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya!

Post a Comment

0 Comments