BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo hili haliepukiki katika safari yako ya mafanikio.

 




Ni kwamba kama unahitaji kufanikiwa lazima ujifunze kudili na kukataliwa (rejection)

Katika maisha yako lazima itatokea watu wakakukataa kabisa. Marafiki watakukataa, wafanyakazi wenzako watakukataa, maombi yako ya kazi yatakataliwa, wateja wa kununua bidhaa zako watazikataa.

Na zaidi Mpenzi uliemwamini ukampa kila kitu, ukajishusha kwake na kukubali kuwa mtumwa wake atakukataa.

Hii ndiyo dunia tuishiyo mimi na wewe yenye kila aina ya rangi, dunia ambayo ina wakatisha tamaa wengi zaidi. Kwenye kila ukifanyacho wapo watu kazi yao ni kushangaa au kutokukubali kwenye kile ufanyacho.

Lakini kama unayo kiu ya mafanikio na unahitaji kufanikiwa lazima ujifunze kudili na huko kukataliwa na kusonga mbele kwa ujasiri mkubwa(ku-move on great passion!)

Hauwezi ukaendelea kuishi maisha ya huzuni, majuto na hofu ya wale waliokukataa, waliokuacha katika wakati mbaya, waliokusaliti na waliokupotezea muda wakati ulikuwa sehemu ya mafanikio yao!

You have let go(Ni lazima uwaache waende) na ku-focus(ujikite) katika kutimiza kusudi la uwepo wako na punde kidogo waliokukataa watakuona uko kileleni (At the top!)

Yesu kristo mwenyewe alisema "Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni" (I.e the stone which the builders rejected is put right at the Top)

Kubali kukataliwa na waashi, na muda si mrefu(soon) utakuwa jiwe kuu la pembeni linalokimbiliwa na si kukimbiwa!

Nilichojifunza kwa miaka yote hii ninayopitia magumu na changamoto fulani fulani katika maisha yangu kiujumla, ni kwamba MUNGU anayo tabia ya kuwabariki watu waliokataliwa.

Hivyo neema ya kimafanikio ipo zaidi kwa wale watu ambao hukataliwa katika jamii yao, huku wao kukataliwa huko hukugeuza kama fursa  ya kupata kile wanachokitaka kwenye maisha yao.

Mungu anayo tabia ya kuwatumia wale watu waliodharauliwa hapo awali kutimiza lengo na kusudi lake,usiogope wewe ni mmoja wa wale waliokubaliwa na Mungu vya duniani visikupe presha na kukutoa kwenye uwepo na baraka za Mungu...

Pambana usikate tamaa hasa pale wanapokukataa watu katika mazingira yako

Ndimi; Afisa Mipango Benson Chonya!

Post a Comment

0 Comments