Unapokwenda kufanya usaili wa ajira huwa kunakuwapo na maswali mbalimbali ambayo kimsingi mtahiniwa wa maswali hayo anapaswa kujianadaa vyema katika kuyajibu maswali hayo vyema hatimaye aweze kupata ajira aitakayo.
Miongoni mwa maswali ambayo utaulizwa ni pamoja na suala la mshahara. Hivyo kama mtahiniwa ni lazima ujiandae vyema kujibu swali hili kwa sababu ni miongoni mwa maswali ambayo hayaepukiki uwapo katika chumba cha usaili.
Unapoingia kwenye chumba cha usaili yapo maswali mengi ambayo utaulizwa kama nilivyosema hapo awali. Unapoulizwa ni kiasi gani cha mshahara unachotaka tukulipe?.
Hapa unachoshauriwa ni kwamba usijibu tu majibu ambayo yatakuja kinywani mwako bali unatakiwa kuwa ulikwisha fanya utafiti wa awali ni kiasi gani cha mshahara ambacho watu wanaofanya kazi kama yako uliyoiomba huwa wanalipwa.
Mara nyingi wajiri wengi huwa wanapenda kuuliza swali hili ili kujiridhisha vya kutosha kutoka kwako kama unaijua vyema kampuni husika au kukupima wewe kama pindi watakapokuajiri utawaibia ama laaah.
Yupo rafiki yangu wa miaka mingi alikwenda kufanya usaili sehemu fulani ila alipoulizwa ni kiasi gani unataka tukulipe, rafiki huyo kwa kuwa alikuwa hajafanya utafiti wa kutosha kutoka kampuni husika kwamba ni kiasi gani huwa wanalipa basi yeye alisema anaombwa alipwe shilingi laki saba.
Alijibu anataka kulipwa laki saba, wakati huo kampuni hiyo ilikuwa ina uwezo wa kumlipa mshahara wa shilingi la tatu. Mara baada ya kujibu hivyo mtu huyo alikosa kazi husika kwa sababu mwajiri aliona kuna gepu kubwa la uwezo wake wa kumlipa.
Pia mwajiri aliamini kama endapo atamlipa kiasi kile cha shilingi laki tatu wakati mhusika anataka laki saba basi mtu huyo ni lazima angemuibia tu ili kufidia kiwango cha laki saba kile alichokisema wakati wa asaili.
Kwa kuona mfano huo, nawe unapokwenda kuomba kazi mahali fulani ni lazima ujue ni kiasi gani cha mshahara ambacho huwa wanalipwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye kampuni aliyoomba ajira.
Kama wewe ni mtalamu wa usafi, mtalamu wa mahesabau au kazi yeyote ile ni lazima ufanye uchunguzi wa kutosha kujua wafanyaazi waliokwisha kuajiriwa kwenye kampuni husika huwa wanalipwa kiasi gani.
Ukisha jua ni kiasi gani wanalipwa pindi uwendapo kwenye usaili wa ajira unatakiwa usizidi kiwango kikubwa cha mshara ambacho utaulizwa. Kama ulifanya utafiti kisha ukajua wafanyakazi huwa wanalipwa laki tatu basi wakikuliza ni kiasi gani cha mshahara unataka tukulipe basi unaweza ukasema kama ikiwapendeza kwangu naona kiasi cha shilingi laki mbili na themanini kinanitosha vyema.
Ni vyema kujishushia kiwango cha mshahara kwa sababu ni rahisi sana kwa mwajiri husika kuona anao uwezo wa kukulipa kuliko kutaja kiwango kikubwa cha mshahara ambacho ni kikubwa kitakachomfanya mwajiri ashindwe kukulipa hatimaye kujikosesha kazi husika.
Ukiyazingatia hayo itakusaidia sana kuweza kupata ajira uipendayo kiurahisi.
Ndimi Ofisa Mipango; Benson Chonya.
.jpeg)
0 Comments