BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Fursa si pesa, fursa ni zaidi ya pesa.

Tunapozungumzia fursa, kitu cha kwanza kinachokuja akilini mwa wengi ni kuwaza pesa, yaani mafanikio ya pesa yatakayopatikana kutokana na fursa hiyo. Wengi wanajua, maana ya fursa ndio iko hivyo.

Lakini hata hivyo fursa si pesa tu. Tunaposema fursa ya kufanya jambo fulani mbali na pesa kuna faida nyingine nyingi ambazo huwa zinapatikana. Kwa mfano, kuna faida ya kukua, uzoefu, kujiboresha na kufanikisha.

Kila siku tunasema ni siku iliyojaa fursa hatumaanishi pesa tu, bali pia kuna fursa za kuwapa watu moyo, kuwafariji, kuwafurahisha na kuwapa watu mwelekeo wa maisha yao kwamba kesho inawezekana.

Je, unatumia fursa za kila siku kuwasaidia wengine au bado una mawazo mgando fursa ni pesa tu. Ondokana na mawazo hayo fursa si pesa pekee, fursa ndani yake ina mambo mengine mengi na yenye msaada mkubwa.

JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYA, fursa si pesa tu, ni zaidi ya pesa. Kwenye fursa sio ipo pesa peke yake, kuna mambo mengine yanayoendana na pesa. Acha kuwaza fursa ni pesa tu peke yake, utajikwamisha.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments