Mahitaji:
1.
Unga wa dengu ½ kilo
2.
Unga wa pilipili binzari nyembamba
½ kijiko cha mezani
3.
Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha
chai
4.
Unga wa mchele ¼ kilo
5.
Chumvi kiasi
6.
Mafuta ya alizeti ½ lita
7.
Baking powder
Namna ya kutengeneza
Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa
dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa
binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo
kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi.
Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu
saa hadi saa moja.
Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka
jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia
tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi
kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha
mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye
sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Ikiwa huna mashine, unaweza kutumia bakuli ya
bati iliyotobolewa mfano wa chujio. Na kisha kandamiza kwenye tundu hizo hadi
unga wako upite kwenye tundu za bati hilo na kufanya kama nyuzi nene na ndefu.
Fanya kama nilivyoelekeza hapo juu.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya kwa msaada wa
mtandao.
0 Comments