Mahitaji
1. Maembe 3 makubwa
2. Mtindi wa vanilla au wa kawaida vikombe 5
3. Sukari kiasi chako
Namna ya kutengeneza
Menya embe katakata vipande vidogo vidogo na mimina katika blender. Weka na Mtindi na Sukari. Saga mpaka iwe laini kabisa. Mimina mchanganyiko katika vikopo vya ice cream. Gandisha katika freezer muda wa masaa 6 au 8. Baada ya hapo lamba lamba za embe tayari kuliwa.
Imeandikwa na Benson Chonya kwa msaada wa mtandao.
0 Comments