Kati ya kitu ambacho huwezi kukwepa katika safari ya mafanikio yako ni changamoto. Kwa namna yoyote ile ni lazima utaweza kukutana na changamoto, uwe unataka au hautaki, utakutana nazo.
Na ili kushinda changamoto yoyote ile, unahitajika uwe na ufahamu au uelewe mambo matatu ya msingi sana kwako. Kama hautaelewa hayo mambo matatu haiwezekani kushinda hiyo changamoto.
Jambo la kwanza, muda.
Ili uweze kuishinda changamoto yako, lazima ujipe muda. Haiwezekani changamoto imetokea sasa hivi, na unataka kuishinda muda huu huu, hicho kitakuwa ni kitu kigumu na sio rahisi. Muda unatakiwa ili kushinda changamoto.
Jambo la pili, juhudi.
Pia mbali na muda inahitajika, juhudi. Ni lazima uweke juhudi sana ili kushinda changamoto yako. Ikiwa utaiendea changamoto yako huku ukiwa unacheka cheka, basi ni ngumu kuishinda changamoto yako. Unatakiwa uweke juhudi haswa ili kushinda.
Jambo la tatu, nguvu.
Unatakiwa uelewe, kuna changamoto ambazo ili kuzitatua, zinahitaji uwekeze nguvu pia. Inawezekana kuna kazi unatakiwa uifanye, sasa kwa kufanya hivyo utaishinda changamoto yako.
Hayo ndio mambo unatakiwa kuyajua na kuyazingatia ili uweze kuishinda changamoto yoyote. Kama usipoyajua mambo hayo huwezi kufanikiwa katika kushinda changamoto yako.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments