Kwa chochote unachokipenda na kukithamini, kifanyie kazi kitu hicho. Weka juhudi kwenye kile unachokipenda na weka upendo kwenye juhudi zako. Kama hakuna juhudi, upendo unakuwa kidogo au hakuna kabisa. Kama hakuna upendo na kujitoa nyuma yake, juhudi zako zote zinakuwa sawa na kazi bure.
Unapokuwa unaipa thamani na kuipenda kazi yako, hakuna kitu cha kuweza kukuzuia kufanikiwa. Kuweka juhudi na upendo kwa kile unachokifanya ni kitu cha muhimu sana ili kufikia mafanikio makubwa.
Elewa katika kila juhudi, kuna changamoto, lakini kwa kuwa ndani yako una upendo wa hicho ukifanyacho, changamoto hizo haziwezi kukuzuia kitu chochote. Kuwa na mtazamo wa kupenda kile unachokifanya, na ukikipenda tu, juhudi lazima utaweka bila kulazimishwa.
KITU CHA KUZINGATIA NA KUELEWA, kila wakati weka juhudi na weka upendo kwa kile unachokifanya, utafanikiwa. Juhudi na upendo wa kufanya kile unachokipenda toka moyoni, huwa vinazalisha mafanikio makubwa wakati wote
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments