BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ufanisi Mkubwa Unakuja Hivi...

Kukubali jinsi jambo lilivyo au jinsi lilivyokuja kwako, kunakufanya wewe uweze kutenda kwa ufanisi. Pia ufanisi unakufanya wewe kufanya jambo ulilolikubali kwa usahihi.

Unapokubali uhalisia wa mambo jinsi ulivyo, unaweza kubadili chochote na kukifanya kwa ufanisi mkubwa. Ipo hivyo kwa sababu, umekubali hali halisi, hivyo, ufanisi lazima uuweke tu.

Kama unajijua una ufanisi wa kubadili mambo, basi elewa kwanza umekubali mambo hayo kwa jinsi yalivyo. Kukubali na ufanisi ni vitu ambavyo vinaenda pamoja kimafanikio.

Chochote ambacho kimetokea tayari kimetokea. Chochote ambacho kimesemwa tayari kimeshasemwa, inakubidi ukubali kama kilivyo na tafuta jinsi ya kukifanya kwa ufanisi tu.

Acha kutumia nguvu zako nyingi kubishana na uhalisia jinsi ulivyo. Weka ufanisi wako kwa ambacho tayari umeshakubali. Ukikubali, utaweka umakini na ufanisi wako wote hapo.

Ufanisi mkubwa unakuja na wewe kukubali hali jinsi mambo yanavyokuja au kutokea. Hata hivyo,  kukubali huko haimaanishi wewe ni dhaifu bali ni kutafuta kuwajibika zaidi.


Post a Comment

0 Comments