Ikiwa nia yako ni kuumiza wengine, basi hata wewe itafika muda utaishia kuumia kama hao wengine unaotaka kuwaumiza.
Ikiwa nia yako ni kubabaisha, basi hata wewe ni rahisi kuishia kwenye kudanganya danganya ili kupata hicho ukitakacho.
Ikiwa nia yako ni kutoa kwa wahitaji, basi utajikuta na wewe unapokea kama vile utoavyo kwa hao watu wengine.
Ikiwa nia yako ni kufundisha wengine, basi utajikuta unajifunza mambo mengi sana ya kukusaidia pia kimaisha.
Ikiwa nia yako ni kuwakubali wengine, basi utajikuta unaheshimika sana na hao unaowakubali na wengine pia.
Ikiwa nia yako ni kusaidia watu, basi utajikuta unasaidiwa na watu wengi pia kwenye maisha yako bila hata kutegemea.
Ikiwa nia yako ni kufanya maisha ya wengine kuwa ya mafanikio na bora, basi na wewe maisha yako yatakuwa bora vivyo hivyo.
Hauwezi kuikwepa nia yako, hata kama nia hiyo inaenda kwa wengine, lakini nia hiyo uliyonayo itakurudia pia wewe.
Nia yako ni lazima irudi kwako, iwe kwa kufanya maisha yako yaende mbele au yarudi nyuma, lakini nia uliyonayo itakurudia tu.
Unatakiwa ujue nia yako ndio inaamua wakati mwingine ule ubora wa maisha yako, inategemea na nia uliyonayo.
Kila wakati jitahidi uwe na nia nzuri, hiyo kwa sababu kila nia yoyote ile uliyonayo muda ukifika ni lazima itarudi kwako.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia
WhatsApp.
0 Comments