BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hofu Yako Ipo Hapa...

Hata siku moja, huwezi kwenda dukani na kununua hofu. Pia hofu huwezi kuichimba chini. Hofu haiwezi kutengenezwa kiwandani au kutengenezwa katika maabara. Hofu haifichiki juu milimani au katika bahari.

Siku zote tambua hofu yako ipo tu akilini mwako. Wewe ndio mwenye maamuzi unatawala vipi hofu hiyo uliyonayo akili mwako au hofu hiyo itakutawala na kushindwa kufanya kitu chochote kile ukitakacho.

Hofu uliyonayo unajitengenezea wewe na unaweza kuwa nayo au kutokuwa nayo kama ukiamua. Unaweza kuitupa hofu yako au ukabaki nayo, ingawa kubaki na hofu kwako itakuwa na madhara makubwa na itakukwamisha. 

Mara nyingi hofu zako unajitengenezea mwenyewe. Usijaribu kutumia hofu ikuzuie kufanikiwa,  bali itumie kusonga mbele na si kukurudisha nyuma. Hofu unaweza kuitoa ukiamua, maana ipo akilini mwako.

Jiulize una hofu? Kama unayo hofu yoyote, weka mikakati ya kuitoa hofu hiyo. Kama unayo itumie ikusaidie kufanikiwa zaidi. Usiitumie hofu kukufanya ukashindwa kuchukua hatua. Hofu isiwe kikwazo kwako.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.

Post a Comment

0 Comments