Somo la fedha ni la muhimu sana kwa kila mmoja wetu, hii ni kwa sababu tunashindwa kupata au kudumu katika mafanikio yetu hii ni kwasababu hutuna uelewa wa kutosha katika suala la kipesa.
Wengi hatuelewi namna ya kupata pesa na namna ya kuzifanya pesa hizo ziendelee kuwa upande wetu, Ila ukweli unabaki palepale siku zote kwamba, ukitaka kufanikiwa kifedha na kufika mbali, unalazimika kujua mambo haya yafuatayo;
1. Jinsi ya kutawala pesa zako.
Katika maisha yako yote unatakiwa kuwa mtalawa wa fedha zako na sio fedha zikutawale wewe. Wapo wengi wetu wanashindwa kufanikiwa kimaisha hii ni kwa sababu fedha zimewatawala wao, yaani unaweza ukaona mtu kapata fedha lakini atataka kila mtu ajue kwamba mtu huyo ana pesa, kitendo hiki ndicho tunachokita kutawaliwa na fedha.
Nini kifanyike.
Jambo muhimu la kuzingatie ni kila mmoja wetu ahakikishe hatawaliwi na pesa ila yeye ndio anayezitawala pesa hizo. Wewe ndiye unayekuwa na maamuzi sahihi juu ya kuzitumia pesa hizo na si vinginevyo.
2. Jinsi ya kutoka kwenye madeni.
Wakati mwingine madeni ni njia namabari moja imfanayayo mtu awe maskini kama hatakuwa makini mtu huyo, japo wapo baadhi ya watu, wao huamini ya kwamba mfanyabiashara wa kweli haogopi madeni, huko ni kujidanya.
Nini kifanyike.
Unatakiwa kuelewa ya kwamba madeni ni mabaya sana hasa ukiwa na hulka ya kujiendekeza katika michezo hii, hivyo kila wakati ili uweze kuwa na uhuru wako binafsi hususani katika uhuru wa kipesa unatakiwa kuondokana na madeni hayo mara moja, kwani madeni ni mabaya sana.
3. Jinsi ya kuongeza kipato.
Mara zote ukitegemea mfereji mmoja kama chanzo chako cha kipato basi fahamu fika maisha yako yatakuwa ni yale yale kila wakati.
Nini kifanyike.
Jambo la muhimu unalotakiwa kulikumbuka hapa ni kwamba kila wakati ni lazima uwaze kuongeza njia mbadala ya kuongeza kipato chako, na miongoni mwa njia zitakazokusaidia kuwa hivyo ni kuongeza wigo wako wa kutafuta pesa, usitegemee njia moja ya kujiingizia kipato.
4. Jinsi ya kuweka akiba na jinsi ya kuwekeza kwa ajili ya baadae.
Wakati mwingine hatufahamu lile litakalojitokeza siku ya kesho hii ni kwa sababu kesho si rafiki kwetu ila tunaamini siku hiyo ipo, kama tuaamini hivyo basi tunatakiwa kujifunza kuweka akiba kwan hatujhi nini kitokea siku ya kesho.
Uwekaji wa akiba ni mzuri hii ni kwa sababu miongoni mwa faida itokanayo na kuweka akiba ni kwamba inasadia kutatua changamoto husika kwa muda muafaka hasa unapokuwa haupo vizuri katika suala la kifedha.
Unachotakiwa kufanya
Ni kuhakikisha kwa kila kipato unachopata unatenga asilimia kadhaa kwa ajili ya akiba hii ni kwa sababu hatuajui likalotokea siku ya kesho.
Hayo
ndiyo mambo ya msingi unayaopaswa kufahamu kuhusu fedha.
Ndimi afisa mipango; Benson Chonya.
0757909942

0 Comments