Mwandishi fulani aliwahi andika katika fasihi andishi akisema, “siraha hatari zaidi duniani si mabomu ya nyukilia kama wengi wanavyodhani, bali siraha hatari zaidi duniani ni hofu”. Hofu ndiyo kitu hatari zadi duniani ambacho kimewafanya watu wengi wafe na uwezo wao mkubwa pasipo kufanya vitu vikubwa ambavyo waliumbwa navyo.
Hofu imesababisha watu wengi waziache fursa nyingi ziwapite mbele ya mawazo na vichwa vyao, hofu imesababisha watu wengi duniani wazidi kuwa maskini kila jua lichomozapo. Wengi wamekuwa waakimini kuwa hawawezi kufanya jambo fulani la msingi kwa sababu ya hofu zilizotawala mioyoni mwao.
Ama hakika, hofu ni rafiki mkubwa wa umaskini katika maisha ya wengi, hivyo ili tuweze kupambana na hali hatimaye kuyafikia mafanikio ya kiwango cha juu yatupasa kuhakikisha na tunapambana kikamilifu ili kuishinda hali hii iliyojengeka ndani mwetu.

0 Comments