Muda unakwenda sana, bila kujali unachukua hatua au hauchuki hatua, lakini muda unakwenda na haukusubiri hata kidogo.
Kwa kuwa muda unakwenda, hutakiwi kulala, ni wakati wa kuchukua hatua na kuamua kuutumia vizuri sana muda wako kwa manufaa.
Uwe umefanikiwa au umeshindwa muda unakwenda, uwe unaishi kwa visingizo au unaishi kwa kuchukua hatua muda unakwenda. Uamuzi ni wako unatumiaje muda wako?
Kati ya kitu ambacho hutakiwi kucheza nacho ni muda, muda ndio maisha yako na muda unakwenda sana, kuwa makini nao ukupe mafanikio makubwa.
Wako rafiki katika mafanikio: Imani Ngwangwalu.
dirayamfanikio@gmail.com

0 Comments