Daima ikumbukwe kwamba mafanikio yako hutokana na vile ambavyo unaitumia siku yako vizuri. Hivyo ulivyo leo ni matokeo ya hatua ambazo ulichukua siku jana. Hivyo yakupasa kuithamani sana siku ya leo kwa sababu ina thamani kubwa sana mbele yako endapo utaamua utachukua hatua stahiki.
Acha kuwa mtu wa kughairisha kufanya mambo ya msingi kwa sababu eti unasema utafanya kesho, kesho siyo rafiki mwema katika kuyasaka mafanikio bali siku ya leo ndiyo yenye thamani kwako.
Watu wote waliowahi kusema kwamba watafanya kesho, asilimia kubwa ya watu hao hawakufanya vitu ambavyo walipanga kuvifanya, Kama umechoka na hali tete ya maisha uliyonayo basi yakupasa kuitumia vyema leo yako ili kuipata kesho yenye furaha na mafanikio tele ndani yake.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
0757909942

0 Comments