Hauwezi kuwa mshindi kila siku na kila wakati kwa kile unachokifanya. Upo wakati kitu hicho unachokifanya kitakupa upinzani au utashindwa kwa namna fulani ambayo hukutegemea. Inapotokea hivyo usife moyo, hiyo ni hatua ya mafanikio pia.
Kila kitu unachokifanya hata kwa mwanzo kikupe mafanikio vipi, elewa ipo siku utakutana na changamoto. Changamoto hizo zinapotokea zisiwe kizuizi kwako cha kukufanya ukashindwa kufanikiwa, bali ziwe daraja kubwa la mafanikio yako.
Wako rafiki katika mafanikio: Imani Ngwangwalu.
dirayamfanikio@gmail.com

0 Comments