BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ukiachana na elimu ya darasani, hii ndiyo aina nyingine ya elimu unayopaswa kuifahamu


Kama leo ningeulizwa ni elimu gani ambayo mtu anaihitaji ili aweze kufanikiwa katika maisha yake, basi mimi ningemjibu muuliza swali, kwamba anahitaji elimu ya utatuaji wa changamto (problem solving) kwa kutafuta majibu sahihi wa changamoto husika.

Elimu ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu pia elimu mtambuka kwa sababu elimu hii inagusa maeneo na sekta zote. Kama unataka kufanya jambo fulani katika eneo lako, basi unatikiwa kuangalia ni tatizo gani linalowakumbuka watu hao kisha wewe ukaleta majibu ya changamoto hiyo. Kwa mfano kama eneo lako lina ukosefu wa maji safi basi, hili ndilo tatizo la eneo hilo basi unachotakiwa kufanya ni kutafuta majibu ya changamoto hiyo.

Elimu hii ya prombem solving ni muhimu sana kwa wale wote wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yao na watu wengine, kwa sababu maisha haya yamejawa na chanagomoto kila sehemu hivyo amua sasa kwa kuamua kuwa wewe ndiye mtafutaji wa majibu wa changamoto hizo. Ukifanikiwa kuliweza suala hilo ni kwamba maisha yako yatabadilikwa sana.

Ndimi afisa mipango, Benson Chonya
mafanikioapp@gmail.com
0747-030303

Post a Comment

0 Comments