Dunia ya leo imejaa maneno
mengi kuliko watu waliopo katika dunia hiyo. Hebu fikiria ya kwamba tafiti za
wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza maneno 16000 kwa siku,
wakati wanaweke wote duniani kwa kila mmoja mmoja huzungumza maneno 25000 kwa
siku, kwa tafiti hizi najaribu kuwaza hivi tuna watu wangapi? Na kila mmoja
akizungumza maneno yake tutakuwa na maneno mangapi?
Najaribu tu kuwaza kwa
sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya watu. Nasema hayo
kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na
katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao
huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyohivyo sawa na kusema.
Hata hivyo maneno ya watu
ambayo yapo katika dunia hii ni yale ambayo yanatengeneza ulimwengu mpya, ulimwengu huo huitwa ulimwengu wa taarifa, katika ulimwengu
huo yapo mengi ambayo utayasema na mengine utayasikia, na katika ulimwengu
hohuo, taarifa hizo hizo ambazo utakuwa unazisikia, yapo yale yatakayokujenga,
lakini yapo yale ambayo yatakufanya uvurugike kabisa.
Na ukweli ni kwamba maneno
ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson hii ni kwa
mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa
zimejaa tarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele
kimaisha.
Na mara kadhaa hali hii hutokea na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye
maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe.
Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho
kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa
wewe jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, tunachotaka
kukwambia siku ya leo ni kwamba acha
kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia kuendesha maisha yako, kwa sababu
kama ukifanya hivyo utaumia sana na utaiona dunia chungu. Hivyo ni vyema ukaamua kuishi wewe kama wewe
kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma kukufanya. Kufanya hivyo itakufanya
uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
Tumalizie kwa sema ya
kwamba endapo utamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza wakatishaji tamaa
katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku zote za maisha yako.
Lakini pia faida nyingine ambazo utazipata pale ambapo utaamua kuishi maisha ya
kujitolea hukumu, utakuwa na uhuru mkubwa katika kutoa maamuzi yako.
Asante sana kwa kuwa
nasi, tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na
uongozi wa mtandao wa dira ya mafanikio na mafanikio App
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya

0 Comments