BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Namna ambavyo historia ya maisha yako inavyoandikwa.

Historia ya maisha yako haiandikwi kwa kalamu. Historia ya maisha yako haindikwi kwa mipango mizuri uliyonayo. Historia ya maisha yako haindikwi kwa sababu wewe unajua kuongea sana. Historia ya maisha yako inaandikwa kwa wewe kuamua kuchukua hatua tena kila siku.

Hatua zako ndizo zitakazoandika historia za maisha yako na si kitu kingine. Uwe umechoka au hujachoka unatakiwa kuchukua hatua. Uwe una hamasa au huna hamasa unatakiwa kujifunza kuchukua hatua. Usiendekeze uvivu maana utakuwa mzigo sana kwako, amua kuandika historia ya maisha yako kwa kuchukua hatua.

Jaribu kufikiri kidogo tu, ni nani ambae aliandika historia ya maisha yake na kubadili maisha yake kabisa kwa sababau tu ya kuongea? Naamini huwezi kumpata mtu wa namna hiyo hata mmoja. Watu wote waliobadilisha maisha yao walichukua hatua na kuamua kupiga kazi kwa uhakika na sio kuongea ongea.

Wako rafiki katika mafanikio Imani Ngwangwalu

dirayamafaniko@gmail.com


Post a Comment

0 Comments