BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Maisha kuwa bora ni matokeo ya mambo haya.



Maisha bora ni matokeo ya kuwa na afya bora. Afya bora imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni afya ya mwili, afya ya akili na afya ya roho. Aina zote hizo za afya zinamsaidia mtu kwa kiwango cha hali ya juu kuwa na maisha bora. 

Sasa tuone faida zitokanazo afya ya mwili, akili na roho kama ifuatavyo;

Afya ya mwili; humsaidia mtu kwa kiwango cha juu kuweza kufanya kazi vizuri tofauti na mtu mgonjwa. Hivyo yakupasa kuzingatia kanuni zote zitakazokusaidia kuwa na afya bora.

Afya ya akili; humsaidia mtu kwa kiwango cha juu sana katika kuwa sawa kiakili, ambapo akili imeubwa na uwezo mkubwa sana wa kiutashi ambapo mtu anatakiwa kutumia vyema akili yake kuweza kupambanua vyema mambo. 

Hivyo yakupasa pia kuitumia akili yako vyema kupambambanua mambo mbalimbali hususani masula ya kujifunza yale yaliyo mema na yenye kukujenga sana kimwili na kiroho ili uweze kufanikiwa zaidi.

Afya ya kiroho; hii ni afya muhimu zaidi ambapo yakupasa kuwa karibu na Mungu wako. Unatakiwa kila wakati kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa sababu kiimani yeye ndiye muweza wa kila jambo kwa kila aaminiye uwepo wake.

Ndimi: Afisa Mipango Bensonchonya

bensonchonya23@gmail.com


Post a Comment

0 Comments