Kuna wakati tunakutana na ugumu sana katika kufanya vile tunavyotaka kuvifanya. Kutokana na ugumu huo na kuna wakati huweza kujikuta hata tukitaka kuahirisha kufanya mambo yetu. Kwa hali yoyote unayokutana nayo hata kama ni ngumu vipi, hebu hicho unachotaka kukifanya kifanye.
Usiahirishe mambo yako kwa sababu ya ugumu, fanya hivyo hivyo, ‘just do it,’. Weka visingizio pembeni, usiwe kama mtoto mdogo ambaye kila kitu anasingizia. Tengeneza ukomavu wa kiakili kwa kuamua kufanya hata kama ipo shida na ugumu vipi wewe fanya kwa kusukuma na utaona mafanikio yakijitokeza kwako.
Wako rafiki Katika mafanikio, Imani Ngwangwalu.
dirayamafanikio@gmail.com

0 Comments