BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kila mafanikio unayoyatamani huanzia katika hatua hii.

Linapokuja suala la kupanga malengo katika maisha yako unatakiwa kuanza na malengo madogo madogo (Baby step). Unaweza ukawa bado hujanielewa ngoja nikuleweshe, ipo hivi kila kitu unachokiona leo hii kimekuwa katika ukubwa huo ambao leo unaouona ni kwa sababu kitu hicho kilianza kwa udogo pia.

Tunafahamu wengi wana ndoto kubwa sana za kuwafanikisha katika maisha yao lakini ni waoga wa kuanzia katika hatua ndogo, kumbuka Unapoanza kufanya jambo  katika hatua ndogo huku ukiweka nguvu na juhudi stahiki katika jambo hilo ni kwamba ipo siku jambo hilolitakuwa kubwa na lenye kukuletea mafanikio makubwa pia. 

Pia unapaswa kukumbuka kuwa maisha ya mafanikio hujengwa na historia, hakuna jambo lilotakalokuwa lenye mafanikio ghafla, kila mtu mwenye mafanikio leo hii ana hstoria yake, historia ambayo inaeleza ni wapi alipoanzia na wapi alipo . 

Hivyo ewe msaka tonge usione aibu kuanza na hatua ya chini katika malengo yako, kumbuka kila safari ya tamu huanza na chachu. Anzia hapo ulipo kuelekea katika safari ya mafanikio yako kwa kuanza na malengo madogo madogo huku ukifukuzia ndoto za malengo makubwa.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya

mafanikioapp@gmail.com

0747-030303


Post a Comment

0 Comments